UTNC.ORG, Union of Tanzanians, North Carolina


Go to content

UTNC Constitution

About Us

KATIBA YA UMOJA WA WATANZANIA NORTH CAROLINA



SURA YA 1: Jina

Jina la chama litakuwa ni UMOJA WA WATANZANIA NORTH CAROLINA “UTNC”


SURA YA 2: Lengo

Lengo la chama ni kuboresha maisha ya mtanzania mkazi wa North Carolina kiuchumi, kielimu, kiafya, kijamii na kitamaduni.

Chama cha UTNC kama UMOJA WA WATANZANIA NORTH CAROLINA si chama cha kisiasa, kidini, kiserikali wala biashara.

SURA YA 3: Uanachama

Sehemu ya 1; Sahili ya uanachama

Lazima awe mtanzania na mkazi wa North Carolina.


Sehemu ya 2; Upendeleo

Lazima akamilishe hatua za uombaji, kuhudhuria mikutano, kulipa ada n.k.


Sehemu ya 3; Aina za uanachama

Chama kitakuwa na tabaka na tapo za uanachama, tabaka za uanachama ni mwanachama hai (rejea sura ya 3, sehemu ya 2) na mwanachama mfu (rejea sura ya 3, sehemu ya 4). Na tapo za uanachama ni kama zifuatazo;

A-Familia

B-Mtu mzima


Sehemu ya 4; Kupoteza uanachama

Upotezaji wa uanachama unatokana na kutohudhuria mikutano, kutolipa ada, kutokamilisha kwa maombi kusimamishwa na mkutano mkuu kwa kupigiwa kura. Theluthi mbili za kura zinatosha kufanya au kupitisha maamuzi yoyote ya chama. Uongozi unaweza kutafakari zaidi mahudhurio ya mwanachma.

SURA YA 4: Ofisi

Sehemu ya 1; Uongozi

Uongozi wa kamati mwenyekiti, mweka hazina, mweka hazina msaidizi, katibu mkuu,na katibu msaidizi n.k.


Sehemu ya 2; Wajumbe wa uongozi

Wajumbe wa uongozi ni lazima wawe si chini ya watano (5) na katika mfumo wa namba witiri.


Sehemu ya 3; Namba za ofisi

Namba za ofisi zitategemea na wingi wa kazi za chama. Bodi inayo uwezo wa kuunda kamati ndogo ndogo za utendaji. Wenyeviti wa Kamati ndogo ndogo wanaweza kuchaguliwa na bodi au kuchaguliwa na mkutano mkuu. Wajumbe wa kamati ndogo ndogo wanaweza kupendekezwa na viongozi wa kamati na kupasishwa na uongozi. Uongozi unao uwezo wa kuchagua wajumbe wa kamati ndogo ndogo. Mkutano mkuu pekee ndio wenye uwezo wa kubatilisha maamuzi yeyote.


Sehemu ya 4; Muda wa ofisi

Chaguzi zitafanyika kila mwaka (kwa mfano, 06/21/04 mpaka 06/21/05). Chaguzi za kamati ndogo zitafanyika wakati wowote zinapohitajika. Kiongozi yeyote katika nafasi yeyote anaweza kugombea tena wakati wewote wa uchaguzi.


Sehemu ya 5; Mamlaka na majukumu

Kazi za uongozi ni kufanya maamuzi muhimu ya chama yasio pingamana na katiba. Maamuzi yote yatakayo husiana na fedha yatafanywa na ofisi ya hazina. Maamuzi yeyote ya matumizi ya fedha yatahitaji sahihi mbili ya mwenyekiti na ofisi ya hazina. Ofisi ya katibu ndiyo itakayo andaa vikao vyote vya chama. Kuanzia wanachama watatu (3) wanaweza kuomba kuitishwa kwa mkutano wa dharura. Uongozi utayatafakari maombi hayo na kuamua. Ofisi ya katibu ndiyo itakayoitisha mikutano ya dharura. Uongozi unao uwezo wa kuvunja kamati ndogo ndogo wakati wewote kwa kupiga kura. Kazi za kina za uongozi zitawekwa wazi na sheria za utendaji.


Sehemu ya 6; Uteuzi na uchaguzi

Kipengele cha 1)Kusahili kugombea

Ili usahili kugombea nafasi yeyote ya chama lazima uwe mwanachama hai (rejea sura 3 sehemu ya 2). Upigaji kura utakuwa Ima wa siri au wa kunyoosha mikono. Watakao weza kupiga kura ni wanachama.



Kipengele cha 2:Uteuzi

Uteuzi utafanyika kwa faida maalumu ya chama na pale tu inapobidi. Uteuzi wa wajumbe maalum wa uongozi utafanywa na mkutano mkuu.

SURA YA 5: Mapato ya chama

Chama kitajiendesha kwa kutegemea miradi, michango na misaada.


Sehemu ya 1; Usimamizi

Ofisi ya hazina ndiyo itakayo husika na uandaaji na usimamizi wa miradi. Usimamizi wa kukusanya michango na misaada ya chama.

Ofisi ya hazina ndiyo itakayo husika na uhifadhi na utoaji rekodi zote za matumizi ya chama.


Sehemu ya 2; Vyanzo vya mapato

Vyanzo vya mapato ni miradi, michango na misaada. Chama kitaandaa miradi yake kwa wanachama na wasio wanachama. Kwa makampuni, mashirika, wafanyabiashara na watu binafsi, chama kitakuwa na aina tatu za michango, nazo ni;



A-Michango ya kuombea uanachama (mara moja) nayo ni $20.00 kwa mtu mzima na kwa familia ni $30.00

BE-Michango ya kila mwezi nayo ni $5.00 kwa mtu mzima na $7.5 kwa familia.

CHE-Michango ya kichwa (malipo ya hatua au adhabu)

SURA YA 6: Mwenendo wa chama

Mikutano mikuu itafanyika si chini ya mmoja (1) kwa mwaka. Mikutano ya uongozi itafanyika si chini ya sita (6) kwa mwaka.

SURA YA 7: Marekebisho ya katiba

Mwanachama yeyote anayo haki ya kupendekeza marekebisho ya katiba. Mapendekezo yeyote lazima yapitiwe na uongozi kabla hayaja pelekwa kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Mkutano mkuu pekee ndio unao uwezo wa kurekebisha katiba.
SURA YA 8: Mapasisho ya katiba

Mkutano mkuu ndio utakao pasisha katiba kwa kupiga kura.


Home Page | About Us | Events | Links | Projects | Summit | Site Map


Sub-Menu:


Back to content | Back to main menu