UTNC.ORG, Union of Tanzanians, North Carolina


Go to content

Projects

Projects

UNION OF TANZANIANS NORTH CAROLINA

MALENGO NA UTENDAJI WA MWAKA WA MAENDELEO

2010-2012

UTNC inakusudia kuleta maendeleo na mabadiliko bora katika jamii ya Watanzania North Carolina,muongozo wa malengo ya Jumuiya ni;


1.Kuunda, kuimarisha na kukuza njia za mawasiliano kati ya Uongozi na Wanajumuiya,Jumuiya ya UTNC na Jumuiya zinazifungamana kikatiba na Jumuiya nyingine za Watanzania Marekani.

" barua pepe
" text group
" Tovitu
" P.o.Box

2.Kukuza mfuko wa chama, Lengo la mwaka wa 2010-2012 ni $25,000.00

" Kushinikiza malipo ya ada na michango
" Kuandaa miradi
" Kutafuta wafadhili
" Kuwashawishi wafanya biashara kutangaza biashara zao kwenye tovitu ya
UTNC

3.Kuandaa njia za kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa;

" kuwashirikisha Watanzania wa NC katika ukusanyaji na utoaji misaada
(Mfano;vitabu,computers,nguo,vifaa vya hospital etc)
" Kuwashirikisha Watanzania wa NC katika huduma za dharura
" Umoja wa Tanzanians kuwa wawakilishi wa Tanzania
" Umoja wa Watanzania NC kuwa daraja la misaada kwa Tanzania


4.Kuandaa njia za Watanzania North Carolina kufaidika na Tanzania

" Kushirikishwa kwa Watanzania NC katika uwekezaji Tanzania
" kupewa taarifa na elimu sahihi ya uwekezaji
" Kuwekewa nafasi maalum za uwekezaji
" Kupata taarifa za vyanzo na Nyanja za maendeleo Tanzania

5.Kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kijamii North Carolina

6.Kusimamia Shughuli za kawaida za kila mwaka za chama;

Marejeo ya Katiba

" Kurejea malengo ya chama
" kuweka wazi mipaka ya chama
" Uongezaji wa aina za Uanachama
" Marejeo ya mfumo mzima wa ada
" Sheria za utendaji
" Aina za Uanachama
" Tahfif ya ada kwa mwanafunzi

Kurejea miradi iliyokwisha anzishwa au jadiliwa

" Ununuzi wa bima ya maisha
" Afya bora na UTNC
" Ukusanyaji wa ada
" Kufatilia madeni ya Jumuiya
" Ukarabati wa Tovitu
" Kukuza mawasiliano na Watanzania wa Charlotte na Raleigh n.k.
" Kutofautisha kati ya wanachama hai na mfu na faida zake
" Kuandaa sherehe za Jumuiya
" Kuandaa kalenda ya mwaka
" Utumiaji wa email za chama
" Suluhu ya account ya chama
" Ufungaji wa website moja
" Malengo au makusudio ya ulipaji ada

Sikukuu zinazotambuliwa na kuazimishwa na Jumuiya ni;

" Sikukuu ya Muungano Zanzibar
" Sikuukuu ya Iddi El'Fitr
" Sikukuu ya Uhuru Marekani
" Sikukuu ya Christmass
" Sikukuu ya kuzaliwa UTNC
" Sikukuu ya Uhuru Tanzania
" Sikukuu ya Mwaka Mpya
" Siku ya Watoto wa UTNC





Home Page | About Us | Events | Links | Projects | Summit | Site Map


Back to content | Back to main menu