About Us
Union of Tanzanian North Carolina ilianzishwa rasmi 2004 na kusajiliwa mwaka 2005, kama Non-Profit Organization .Umoja huu umeundwa kwa lengo la kumnufaisha Mtanzania mkazi wa North Carolina na marafiki, kiafya, kiuchumi, kielimu, kitamaduni na kijamii. Kujenga uwakala bora wa nchi ya Tanzania katika jimbo la North Carolina. Kushiriki katika maendeleo ya kijamii, Na kuimarisha mila na desturi za Kiswahili.
Muongozo wa UTNC unasimamiwa na Katiba iliyosajiliwa chini ya Katibu ya Serikali ya jimbo la North Carolina.
UTNC ni Jumuiya isiyo ya kidini, kisiasa, kikabila, kibiashara, kirangi wala kijinsia. UTNC imekusudia kukuza mahusiano na Jumuiya zinazofungamana kikatiba.